WOSIA KWA WANANDOA by Ferdinand Majimbo
NDOA ni kuvumiliana na bila uvumilivu ndoa haiwezi kufaulu. Kuvumilia kunamaanisha kukubali hali mbaya na ngumu ambazo hazifurahishi mtu. Hasa, hali hizi huwa ni ngumu na nzito sana zinazoumiza mtu. Ni hali ambazo mtu huwa hakuwa amezoea kabla ya kuingia katika ndoa au kutarajia kupata katika ndoa. Baadhi ya shida huwa zinasababishwa na mchumba wake au kuzuka kutokana na hali ambazo haziepukikikamwe. Mtu pia anaweza kusababisha hali ngumu katika ndoa […]